0
WANANCHI wa vijiji vya Manga,Kibasuka,Matongo na Kemambo wilayani Tarime ambavyo vinakusudia kupata uwekezaji mkubwa wa kilimo cha mashamba makubwa ya miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari,wapinga madai ya kwamba wameporwa ardhi yao bila kuwashirikisha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara ya vijiji vilivyomo kwenye Kata hizo,wananchi hao wamesema walifuatwa na watumishi wa serikali wanaosimamia masuala ya ardhi na kuzungumzia masuala ya matumizi bora ya ardhi na masuala ya uwekezaji na yapo mambo ya msingi ambayo walikubaliana.

Wamesema baada ya kuzungukia maeneo yote yanayokusudiwa kufanyiwa uwekezaji wa kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari,yapo maeneo ambayo yalitengwa kwaajili ya malisho ya mifungo hya wananchi,ujenzi wa zahanati na masuala mengine ya kijamii na kinachosubiliwa ni kukutana na muwekezaji.

Katika Kijiji cha Weigita,wananchi hao walidai hawajaona watu waliovamia maeneo yao na wanachokijua kwa sasa wanamsubili mwekezaji ili waje wazungumze nae na kukubaliana masuala ya msingi ambayo pia yatawasaidia kwenye Kijiji chao.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Marwa Ryoba,amesema wao wanakubaliana na masuala ya uwekezaji na wanahitaji kiwanda cha sukari kijengwe kwenye Kijiji chao ili waweze kupata fursa mbalimbali kutokana na uwekezaji.


Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Kisaka ambapo pia ni moja ya maeneo ambayo yamelengwa kufanyiwa uwekezaji wa kiwanda cha sukari wamekana kuporwa ardhi na kudai wanamsubili muwekezaji ili wazungumze nae na kuomba kiwanda kijengwe kwenye eneo lao baada ya kumalizika kwa taratibu zote.

Wamesema mazungumzo yanapokuwa yanaendelea kuache kufanyika upotoshaji na baadhi ya wanasiasa kwa kuamini makubaliano yatafikiwa kwa pande zote kukubaliana masuala ya msingi lakini kwa sasa sio vizuri kuzungumza upotoshaji kwa kuwa itawakimbiza wawekezaji.







Post a Comment