0
MKUU wa Wilaya ya Tarime,Glorious Luoga,amewataka watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuwafatilia waajiri wasiozingatia sheria na kushindwa kuwasilisha michago ya wafanyakazi kwa muda muafaka.

Akifungua kikao cha wadau wa mfuko huo kwenye ukumbi wa CMG wilayani hapa,amesema wapo waajiri ambao kwa makusudi wanashindwa kuwasilisha michango hiyo licha ya kukata kwenye mishahara na kutaka nguvu iongezwe katika suala la kuhakiki na kukagua kuona kama waajiri wanatimiza wajibu wao.

Amesema licha ya kwamba watumishi wa NSSF kuwa wachache wilayani Tarime lakini ni vyema kujipanga kwa kuwa wilaya hiyo ina waajiri wengi ambao wapo ambao wanashindwa kabisa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao.


Mkuu huyo wa wilaya amesema yapo maeneo kama wafanuakazi waa kwenye mahoteli wamekuwa wakinyanyasika na kushindwa kuwekewa akiba kwenye mifuko ya jamii hivyo kutaka eneo hilo pia liangaliwe huku pia akiahidi yeye wenyewe kufatilia katika upande wa wafanyakazi wa mahotelini kuona utekelezaji wake.


“Najua watumishi wa NSSF mpo na sheria mnayo wafatilieni waajiri kwenye maeneo yao kuona kama wanatimiza wajibu wa kuwasilisha michango na kusajili wafanyakazi wao ili katika maisha ya baadae wasiweze kuangaika mara baada yakutoka kazini.


“Nawaomba waajiri mliopo hapa mhakikishe mnazingatia sheria na kuwasilisha michango ya wafanyakazi wenu……najua na nyie meajiliwa hivi mtajisikia vizuri pale mlipo ajiliwa kisha mkashindwa kuwekewa akiba,”amesema Luoga.


Meneja wa NSSF wilaya ya Tarime,Mussa Madadi,amesema katika kipindi cha kuanzia januari hadi mei 2007 waliwafikisha Mahakamani waajiri 6 ambao walishindwa kuwsilisha michango ya wafanyakazi wao kwa mujibu wa sheria.


Amesema jumla ya shilingi milioni 312 zilikuwa zinadaiwa kwa waajiri hao ambapo shilingi milioni 202 zimelipwa baada ya kufikishwa Mahakamani kwa kuwa ilifika mahala waajiri hawakuonyesha dalili ya kulipa kabla ya kufikishwa kwenye Mahakama.


Baadhi ya waajiri walioshiriki kikao hicho wamesema mpango waliouanzisha NSSF katika kukaa pamoja na kujadiliana itasaidia kukumbusha katika suala la uwasilishaji wa michango ya wafanyakazi na kuzungumzia changamoto mbalimbali baina ya mfuko na wadau.


Wadau wakifatilia kikao hicho
 Meneja wa NSSF wilaya ya Tarime akizungumza kwenye kikao hicho
 Wadau wakiendelea kufatilia






 Meneja wa NSSF mkoa ewa Mara,Mvungi Chayoa,akizungumza kwenye kikao hicho cha wadau
 Ufatiliaji
 Mkuu wa wilaya akitoa maelekezo

Mkuu wa wilaya na wadau
 Mkuu wa wilaya ya Tarime katika picha ya pamoja na watumishi wa NSSF wilaya ya Tarime


 Mkuu wa wilaya akiagana na meneja wa mkoa mara baada ya kufungua kikao hicho
 Akiagana na meneja wa wilaya


Post a Comment