SHIRIKA la
Madini la Taifa(Stamico) limekusudia kuendelea na mipango mbalimbali yenye
lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwafanyia
tafiti kwenye maeneo yao ya uchimbaji ili waweze kuchimba kwa tija.
Kauli hiyo
ilitolewa na Meneja wa Uchimbaji Mgogo wa shirika hilo,Tuna
Bandoma,alipotembelea mradi wa kituo cha mfano cha utafiti na mafunzo kwa
wachimbaji wadogo Buhemba kuangalia
shughuli za utafiti zinavyoendelea kwenye eneo hilo.
Alisema
shirika ni walezi wa wachimbaji wadogo kuhakikisha wanafanikiwa kwenye
shughulizi zao na kuweza kulipa kodi stahiki hivyo kuweza kuchangia katika pato
la taifa na kuimalisha uchumi kwenye familia zao.
Bandoma
alisema kwa kipindi kirefu wachimbaji wdogo wamekuwa wakikabiliana na
changamoto mbalimbali ikiwemo kutumia nguvu nyingi kuchimba bila ufanisi na
kuja kwa mradi huu ni mafanikio makubwa kwa wachimbaji hao.
Alisema
kupitia mradi huo ambao unafanyika kwenye maeneo 6 ya awali hapa nchini utatoa
taarifa za kibailojia ambazo zitasaidia kutambua maeneo ambayo dhahabu na
madini mengine yanapatikana hivyo kupelekea wachimbaji kuchimba kwa ufanisi.
“Uzalishaji
wa wachimbaji wadogo na namna ya kusaga dhahabu tumebaini dhahabu nyingi
inapotea na mradi huu unakuja kuwasaidia wachimbaji wadogo na pia yapo matumizi
ya kemikali isivyo stahili yote hayo mradi huu utakuja kuyamaliza yote hayo,”alisema
Bandoma.
Kwa upande
wake Katibu wa Wachimbaji Wadogo mkoa wa Mara,Milele Mundeba,aliishukuru
serikali kupitia Stamico kwa hatua ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kitaalamu
zaidi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Alisema bila
msaada kutoka serikalini wachimbaji wadogo hawawezi kufika popote na kufanikiwa
kwenye shughuli za uchimbaji ili waweze kulipa kodi na kusaidia maendeleo ya
familia ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto shule.
Mjiolojia
mwandamizi kutoka Stamico,Robert Erick,wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha
mradi huo katika eneo hilo la Buhemba na yapo matumaini makubwa ya kupatikana
kwa dhahabu ya kutosha katika maeneo ambayo wameyafanyia utafiti na kuwaomba
wananchi wawe na subira ya kuchimba kwa uhakika.
Meneja Uchimbaji Mdogo kutoka Shirika la Madini la Taifa(Stamico),Tuna Bandoma(katikati),akiwasikiliza wataalam wa bailojia namna kazi ya tafiti inavyoendelea katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kwenye eneo la Buhemba mkoani Mara.
Wataala wakiendelea na shughuli za tafiti
Meneja Uchimbaji Mdogo,akiangalia mawe ambayo yanatarajiwa kufanyiwa utafiti yaliyotolewa kwenye miamba
Katibu wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara,Milele Mundeba,akizungumza na kuishukuru serikali katika kuwasaidia wachimbaji wadogo
Post a Comment
0 comments