MBUNGE wa
Jimbo la Bunda mjini, Ester Bulaya (Chadema) ametoa msaada wa mambo na
vifungashio vyake vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17 ili kuweza kufanikisha upatikanaji
maji kwenye Kata 7 za jimbo hilo.
Akikabidhi msaada
huo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda kwa niaba ya mbunge huyo,
diwani wa Kata ya Bunda stoo, Daud Chiruma, amesema Bulaya ameamua kutumia
fedha za mfuko wa jimbo ili kuweza kukabiliana na tatizo la maji na kupunguza
kero kwa wananchi.
Amesema
katika mji wa Bunda na jimbo hilo kwa ujumla tatizo la maji limekuwa ni kero
kubwa tangia miaka ya nyuma na tatizo hilo limeanza kushughulikiwa na mabomba
hayo yataweza kusaidia kufikisha maji kwenye makazi ya wananchi.
Diwani huyo
amesema msaada uliotolewa na mbunge umepokulewa na wananchi na ni vyema ofisi
ya mkurugenzi ikatumia utaratibu mzuri kuhakikisha mabomba hayo yanapelekwa na
kusambazwa maeneo husika ili wananchi waweze kupata maji kama ilivyokusudiwa.
Akipokea
msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda, Rick Kaduri,
amemshakuru mbunge huyo kwa msaada uliotolewa kutokana na adha ya maji iliyopo
na kuahidi kufikisha msaada huo maeneo husika na kufanyiwa kazi.
Amesema
tatizo la maji ni kero kubwa iliyopo kwenye halimashauri ya mji wa bunda na
kusema wataalamu wa maji katika mji huo watahakikisha wanafanya kazi ya kulaza
mabomba hayo ardhini na kuwafikishia maji wananchi kama ilivyokusudiwa.
Katibu wa
mbunge wa jimbo hilo, Yohana Kaunya, amesema msaada huo ni awamu ya kwanza
itakayohusisha Kata 7 kati ya 14 ambazo ni Nyamakokoto,Bunda mjini,Bunda
stoo,Babalimu,Manyamanyama, Nyasura pamoja na Balili na maeneo mengine
yatafikiwa baadae.
Diwani wa Kata ya Bunda mjini,Kunaga,akichimba mtaro kupitisha mabombaKatibu wa Mbunge,Yohana Kaunya akizungumzia msaada uliotolewa
Diwani wa Bunda Stoo ambaye alikabidhi mabomba kwa niaba ya Mbunge Bulaya
Wananchi wakichota maji kwenye chanzo cha maji Kata ya Bunda Stoo yanayopatikana kwa tabu ambapo msaada wa mabomba utawasaidia
Post a Comment
0 comments