0
WANAFUNZI katika shule ya sekondari Tarime wametakiwa kuzingatia suala la elimu na kuipa kipaumbele ili kuweza kufikia malengo yao ikiwemo kuwa viongozi wa baadae na kuweza kulitumikia taifa kwenye sekta mbalimbali za shughuli za kijamii.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye maafali ya 38 ya kidato cha 4 katika shule ya sekondari Tarime, mkuu wa wilaya hiyo, Glorious Luoga na mbunge wa Jimbo la Tarime mjini, Esther Matiku, wamedai suala la elimu lina umuhimu mkubwa katika kufikia malengo na mafanikio.

Mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maafali hayo,amesema walimu wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali za ufundishaji ili kuwajenga wanafunzi lakini wapo ambao wamekuwa hawazingatii na kupata matokeo ya chini kwenye mitihani.

 Mkuu wa wilaya na mbunge wakibadilishana mawazo




 Wanafunzi wakiimba wimbo wa taifa
 Sehemu ya wazazi wakifatilia maafali hayo
 Risala ya wanafunzi ikisomwa kwa viongozi
 Mbunge Esther Matiku akizungumza kwenye maafali hiyo

 Mbunge akitoa zawadi ya seti ya jezi na mipira kwa timu ya shule
 Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, akizungumza kwenye maafali hayo

Mkuu wa shule ya sekondari Tarime,Mugisha Galibona, akitoa taarifa ya shule

 Zawadi zikitolewa
 Pongezi zikitolewa kwa wahitimu
 Mkuu wa wilaya na mbunge wakisisitiza umuhimu wa elimu kwa wanafunzi


Post a Comment