0
 MKUU wa Wilaya ya Musoma, Dk.Vicent Naano, ameongoza vikosi vya majeshi pamoja na wananchi wa wilaya hiyo na halmashauri 2 za manspaa ya Musoma na Musoma vijijini kuadhimisha kumbukizi ya miaka 18 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kufanya bonanza la michezo na kutoa wito wa kila mmoja kushiriki kufanya michezo kama ambavyo alikuwa akifanya Mwalimu Nyerere kwa kuwa michezo ni muhimu na inafanya mwili unakuwa imara wakati wote
 Mchezo wa netball ulichezwa kwenye viwanja vya dayosisi ambapo timu ya kombaini ya wananchi iliifunga kombaini ya majeshi 28-8

Meya wa manspaa ya Musoma akishangilia ushindi wa mchezo wa netball


 Mchezo wa kuvuta kamba pia ulikuwepo
 Mchezo wa kufukuza kuku ambapo mshindi aliondoka na kitoweo hicho

 Watu wakikimbia na magunia kwenye bonanza hilo
 Viongozi wakijiandaa na mbio za mita 100



 Meya akihamasisha wananchi kuwavuta kombaini ya majeshi ambapo walishinda kwa kuwavuta
 Kikosi cha kombaini ya majeshi ambacho kilishinda 3-1 dhidi ya kombaini ya wananchi
 Kombaini ya wananchi waliofungwa kwenye bonanza hilo



Nahodha wa timu ya kombaini ya majeshi akisalimiana na kamanda wa kikosi cha 27 Makoko baada ya kumalizika kwa mchezo wa soka
Mshindi wa kukimbiza kuku akisalimiana na mkuu wa wilaya

Post a Comment