MKUU wa
Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu, amewashutumu viongozi wilayani humo kushiriki
kuhujumu miradi ya maji ili kuweza kufanya biashara ya miradi yao binafsi na
kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na matatizo ya upatikanaji wa maji.
Kauli hiyo
ameitoa wakati akizindua mradi mpya wa maji wa Rain Tanzania unaofadhiliwa na
Coca cola Africa Foundation na kusimamiwa na Amref ambao kukamilika kwake
utawezesha Kata 4 za wilaya hiyo kunufaika kwa kupata maji safi na salama kwa
wananchi zaidi ya laki moja.
Akizungumza
kwa uchungu akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo wakiwemo
madiwani,watendaji wa Kata,wakuu wa idara na wananchi,mkuu huyo wa wilaya
amesema wapo viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhujumu miradi kwa
manufaa yao binafsi na kupelekea wananchi kuendelea kuumia.
Meneja wa Coca cola mkoa wa Mara, Shabani Mshana akifatilia uzinduzi huo
Meneja mradi wa kutatua kero ya maji (Rain Tanzania) katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Mhandisi Temu Japhet akizungumza kwenye hafla hiyo |
Picha ya washiriki wa uzinduzi huo wakiwa na mkuu wa wilaya ya Serengeti
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Nurdin Babu akizungumza kabla hajazindua mradi huo
Utepe ukikatwa
Viongozi wakifatilia uzinduzi huo
Post a Comment
0 comments