MKUU wa mkoa
wa Mara, Adamu Malima, amewasili kuanza kazi rasmi baada ya kuteuliwa hivi
karibuni kushika nafasi hiyo huku akianza kutoa angalizo kwa watumishi mkoani
humo kwenda na kasi ya maendeleo ili kufikia malengo yanayo kusudiwa.
Akizungumza
na watumishi hao mara baada ya kuwasili kwake,amesema siku zote amekuwa akitaka
kufanya kazi na watu wanaojituma kwenye majukumu yao na kumtaka kila mtumishi
kutimiza majukumu yake awapo kwenye eneo
lake la kazi.
Amesema
mtumishi mzembe na asiyetekeleza majukumu yake hana nafasi ya kufanya nae kazi
kama mkuu wa mkoa ambaye amekuja kusukuma mbele maendeleo ya mkoa.
Malima
amesema kwa mtumishi ambaye anaona hawezi kuendana na kasi ya kusukuma mbele
maendeleo ya mkoa ni vyema akatoa taarifa mapema ya kujiondoa kwenye nafasi
aliyopo kuliko kusubili kuondolewa.
“Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano,Dkt John Pombe Magufuli, imempendeza kuniteua kuja
kumsaidia katika mkoa huu katika kusukuma mbele maendeleo ya mkoa.
“Tutafanikiwa
kufikia malengo ya maendeleo hayo iwapo nyie watumishi mtatenda kazi kwa
kujituma na kutekeleza majukumu yenu ipasavyo na niwaambie wale ambao hawapo
tayari waombe mapema kwa katibu tawala kuondoka kwenye nafasi zao,”alisema
Malima.
Akizungumza
na viongozi wa taasisi mbalimbali za mkoa wa Mara wakiwemo wakuu wa wilaya za
mkoa huo, mkuu huyo wa mkoa amesema katika siku za nyuma kumekuwa na taarifa za
mkoa wa Mara ambazo sio nzuri na haikubaliki kuona matukio hayo yakiendelea
kutokea.
Amesema yeye
ni mtu wa uchumi na mkoa wa Mara unazo fursa nyingi za kiuchumi na kuahidi
kukaa na watu wa takwimu na mfumo wa tehama kuhakikisha taarifa mbalimbali za
kiuchumi zinapatikana zitakazo wasaidia wananchi.
Ameongeza
kuwa anataka mkoa wa Mara pamoja na mambo mengine uwe na wafanyabiashara wengi
wawekeze na kufanya biashara zao ambazo zitaweza kusukuma mbele maendeleo na
kuwaomba viongozi kushirikiana katika kutekeleza majukumu.
Kwa
upande wao viongozi waliohudhuria kikao hicho na mkuu wa mkoa
walimpongeza kwa uteuzi wa nafasi hiyo na kuahidi kufuata maelekezo yake
katika utekelezaji wa majukumu.
RC Malima akisalimiana na watumishi baada ya kufika kwenye maeneo ya ofisiViongozi kutoka wilaya za mkoa wa Mara wakimsikiliza
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tarime,Apoo Cstro Tindwa,(kushoto)akimkabidhi zawadi mkuu wa mkoa
Mkuu wamkoa akionyesha zawadi aliyopewa wilayani Tarime(kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga
Mkuu wa mkoa akisalimiana na mkaziwa Kijiji cha Mrito wilayani Tarime aliyemkuta akichota maji kwenye daraja la mrito akiwa njiani kuelekea wilayani Serengeti
Hapa akiangalia daraja linalotenganisha wilaya za Tarime na Serengeti pamoja na kukagua daraja jipya linalojengwa kwenye eneo hilo
Mkuu wa mkoa akipokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Serengeti
Akisalimiana na wananchi wa Serengeti
Akibadilishana mawazo na wakuu wa wilaya za Serengeti na Tarime
Akizungumza na watumishi wa wilaya ya Serengeti
Akiteta jambo na Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya Serengeti katika kupambana na ukatili wa kijinsia
Hapa anateta na maafisa maendeleo
Baadae alizungumza na Waandishi wa Habari wilayani Serengeti kuzungumzia mikakati yake ya kusukuma maendeleo ya mkoa
Akiteta jambo na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti,Juma Porini(Chadema)ambaye alimpongeza kwa kuhudhuria kikao chake
Makabidhiano ya ofisi na mkuu wa mkoa aliyepita,Dk Charles Mlingwa(kushoto)
Mlingwa akiwaaga wana Mara na kuwashukuru kwa ushirikiano
RC Malima akisikiliza kwa makini
Makabidhiano ya ofisi
Nasaa za Malima
Kuagana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
Post a Comment
0 comments