0



JESHI la polisi mkoani Mara limetoa onyo kwa mtu au kundi la watu watakaotaka kufanya vitendo vya uhalifu katika kipindi hiki cha sikukuu za krismass na mwaka mpya kuwa wataishia mikononi mwa polisi kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha hakuna uhalifu wa aina yoyote utakaofanyika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara,Japhar Mohamed na kamanda wa polisi kanda maalumu Tarime na Rorya,kwa nyakati tofauti wamezungumza na blog hii na kusema wamejipanga ipasavyo ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani sikukuu ya krisimass na mwaka mpya na kuwaomba wananchi kuwapa ushirikiano.

Wamesema katika kipindi hiki sio vyema wanapotoka yumbani kuwaacha watoto pekee yao kwa kuwa wahalifu wanaweza kutumia mwanya huo kufanya vitendo vya uhalifu


 Kamanda wa polisi mkoa wa Mara,Japhar Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake


Post a Comment