0
 WAZEE wilayani Rorya wamelalamika vitendo vinavyofanywa na vijana kwa
kuchukua hatua ya kuwachapa viboko kwa kile kinachodaiwa kuendeleza
mila zisizofaa ambazo pia zimekuwa zikidhalilisha na kuendeleza
ukatili kwenye jamii.

Wakizungumza kwenye semina iliyowahusisha wazee wa mila wa wilaya hiyo
katika kuwashirikisha katika kampeni ya kupambana na ukatili wa
kijinsia hususani wanaofanyiwa wanawake iliyoandaliwa na shirika la
Masister wa Moyo Safi wa Maria Afrika,wamesema maadili kwenye jamii
yamepungua na ndiyo kunapelekea kuendelea kwa vitendo vya ukatili.

Wamesema sio wanawake pekee wanaofanyiwa ukatili bali hata wazee pia
wamekuwa wakifanyiwa hivyo kwa kuendeleza mila za kuwachapa viboko
pale wanapodaiwa kutenda kosa jambo ambalo wamedai linawadhalilisha na
ni moja ya ukatili wanaofanyiwa.

Mmoja wa wazee hao aliyejitamulisha kwa jina la,Andrecus Nyazam, wa
Kijiji cha Kwibuse,alisea zipo taratibu za kufuata pale mtu anapokuwa
amekosa kwenye jamii lakini sio vijana kuchukua hatua ya kuwachapa
wazee viboko kwa kile kinachodaiwa adhabu za kimila.



Amesema mila hiyo ni ya ukatili sawa na ule ambao wamekuwa wakifanyiwa
wanawake kwenye jamii na kudai elimu bado inapaswa kuendelea kutolewa
zaidi ili kuachana na mila ambazo zimekuwa kikwazo katika mapambano ya
kupambana na masuala ya ukatili.

“Tunashukuru kwa semina hii ambayo tumeshirikishwa ili kwa pamoja
tuweze kuimalisha haki za wanawake walio athiriwa na ukatili wa
kijinsia kwenye maeneo yetu lakini na sisi wazee tumekuwa na kilio
chetu cha kudhalilishwa na kufanyiwa ukatili na vijana kwa kuchapwa
viboko.

“Tunakwenda kutoa elimu kwa jamii juu ya kuachana na vitendo vya
ukatili kwenye jamii zetu tunaomba pia sauti zisikike za kukemea mila
zisizofaa ambazo kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha ukatili unaokuwa
unatendeka,”alisema Nyanzam.

Mratibu wa mradi wa kuimalisha haki za wanawake walio athiriwa na
ukatili wa kijinsia unaotekelezwa kwenye Kata 13 za Wilaya ya Rorya,
Nollasko Mgimba, amesema jamii inapaswa kuweka mpango wa kutokomeza
mila ambazo hazifai kwenye jamii na kupelekea ukatili.

Amesema pamoja na ukweli kwamba mila zina umuhimu wake mkubwa katika
jamii lakini kunapaswa kubadilika na kuachana na mila zisizofaa
kulingana na maendeleo ya kijamii hasa katika Nyanja za
kiuchumi,kijamii,kisiasa pamoja na sayansi na teknolojia.












Post a Comment